Revelation of John 11

1Nilipewa mwanzi wa kutumia kama fimbo ya kupimia. Niliambiwa, “Ondoka na ukapime hekalu la Mungu na madhabahu, na wale wanaoabudu ndani yake. 2Lakini usipime eneo la ua wa nje ya hekalu, kwa kuwa wamepewa watu wa Mataifa. Wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.

3Nitawapa mashahidi wangu wawili mamlaka ya kutabiri kwa muda wa siku 1, 260, wakiwa wamevaa magunia.” 4Hawa mashahidi ni miti miwili ya mizeituni na vinara viwili ambavyo vimesimama mbele ya Bwana wa dunia. 5Kama mtu yeyote ataamua kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwadhuru adui zao. Yeyote anayetaka kuwadhuru lazima auawe kwa njia hii.

6Hawa mashahidi wana uwezo wa kufunga anga ili kwamba mvua isinyeshe wakati wanatabiri. Wana nguvu ya kubadili maji kuwa damu na kuipiga nchi kwa kila aina ya pigo wakati wowote wakitaka. 7Wakati watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama anayetoka kwenye shimo lisilo na mwisho atafanya vita dhidi yao. Atawashinda na kuwaua.

8Miili yao italala katika mtaa wa mji mkuu (ambao kimfano unaitwa Sodoma na Misri) ambapo Bwana wao alisulubiwa. 9Kwa siku tatu na nusu baadhi kutoka katika jamaa za watu, kabila, lugha na kila taifa watatazama miili yao na hawatatoa kibali kuwekwa katika kaburi.

10Wale wanaoishi katika nchi watafurahi kwa ajili yao na kushangilia, hata kutumiana zawadi kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nchi. 11Lakini baada ya siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia nao watasimama kwa miguu yao. Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona. 12Kisha watasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni huku!” Nao watakwenda juu mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakitazama.

13Katika saa hiyo kutakuwepo na tetemeko kuu la ardhi na moja ya kumi ya mji itaanguka. Watu elfu saba watauawa katika tetemeko na watakaobaki hai wataogopeshwa na kumpa utukufu Mungu wa mbinguni. 14Ole ya pili imepita. Angalia! Ole ya tatu inakuja upesi.

15Kisha malaika wa saba alipiga tarumbeta yake, na sauti kubwa zilinena mbinguni na kusema, “Ufalme wa dunia umeshakuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake. Atatawala milele na milele.”

16Kisha wazee ishirini na wanne waliokuwa wameketi kwenye viti vya enzi mbele ya Mungu walianguka wenyewe chini kwenye ardhi, nyuso zao zimeinama chini, nao walimwabudu Mungu. 17Walisema, “Twatoa shukrani zetu kwako, Bwana Mungu, mtawala juu ya vyote, ambaye upo na ambaye ulikuwepo, kwa sababu umetwaa nguvu yako kuu na kuanza kutawala.

18Mataifa walikasirika, lakini gadhabu yako imekuja. Wakati umefika kwa wafu kuhukumiwa na wewe kuwazawadia watumishi wako manabii, waamini na wale walio na hofu ya jina lako, wote wawili wasiofaa kitu na wenye nguvu. Na wakati wako umefika wa kuwaharibu wale ambao wamekuwa wakiiharibu dunia.”

Kisha hekalu la Mungu mbinguni lilifunuliwa na sanduku la agano lake lilionekana ndani ya hekalu lake. Kulikuwa na miali ya mwanga, kelele, ngurumo za radi, tetemeko la ardhi na mawe ya mvua.

19

Copyright information for SwaULB